Alhamisi 7 Mei 2026 - 00:10
Mjumbe wa Kundi la Muqawama: Kipaumbele cha leo ni utekelezaji kamili wa usitishaji mapigano

Hawza/ Ali Fayyadh alisisitiza kwamba: Hatutaki kuingia katika mgongano na mamlaka inayotawala, wala hatutaki kuiingiza nchi katika mgogoro wa ndani, ingawa kundi jingine lisilokubaliana na muqawama huenda likajaribu kuisukuma nchi katika mgogoro wa ndani kwa kisingizio cha kunyang'nywa silaha.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Ali Fayyad, mjumbe wa Kundi la Uaminifu kwa Muqawama nchini Lebanon, alitoa hotuba katika hafla ya ukumbusho iliyoandaliwa na Hizbullah kwa ajili ya kundi la mashahidi wa muqawama wa Kiislamu waliouawa kishahidi katika vita vya “Al-Asf al-Ma’kul” wakiitetea Lebanon na wananchi wake.

Hafla hiyo ilifanyika katika Husseia ya Al-Barjawi huko Bir Hassan, kwa ushiriki wa idadi ya shakhsia za wabunge, wanasiasa, watu wa dini, watu wa utamaduni na wanaharakati wa kijamii, pamoja na viongozi wa mitaa, wazee wa eneo na familia za mashahidi, na pia umati mkubwa wa wananchi.

Fayyadh alisisitiza kuwa: Hatutaki kuingia katika mgongano na mamlaka inayotawala, wala hatutaki kuisukuma nchi katika mgogoro wa ndani, ingawa kundi jingine lenye uhasimu na muqawama si tu linapinga, bali huenda pia likajaribu kwa kisingizio cha kuvuliwa silaha kuisukuma nchi katika mgogoro wa ndani. Hata hivyo, kwa tathmini ya uhalisia, kuna njia inayohusiana na utambulisho wa nchi, mustakabali wake, nafasi yake na maslahi yake; njia ambayo bila mjadala na makubaliano ya kitaifa juu yake, tunasukumwa kuelekea humo, na hatutaki kupuuza kwamba Lebanon inasukumwa katika njia hiyo chini ya shinikizo la moto wa mashambulizi ya Israel na vitisho vya Marekani — vinavyowasilishwa kwa jina la “ushauri”.

Aliongeza kusema: Utendaji wa majadiliano wa mamlaka inayotawala una matatizo, ni dhaifu na hauna mwelekeo thabiti, na umejengwa juu ya mantiki ya kuridhia bila kupata faida yoyote au mafanikio. Aidha, kwa uzembe usio wa kawaida, unapuuzia hatari, athari na umuhimu wa kulinda maslahi. Ukosoaji huu si mtazamo wetu tu — sisi ambao tuna tofauti za kimsingi na mamlaka inayotawala — bali pia baadhi ya nchi za Kiarabu na Ulaya zinazounga mkono mazungumzo ya moja kwa moja, nazo zimepinga mbinu ya mamlaka inayotawala katika mazungumzi, zikiwasilisha ukosoaji wa kimsingi na kuonya dhidi ya matokeo ya hatua inazochukua.

Mjumbe huyo wa Kundi la Muqawama alisisitiza kuwa: Kipaumbele cha leo ni utekelezaji kamili wa usitishaji mapigano; kwa maana ya kusitishwa kwa vitendo vyote vya uadui na uharibifu wa kimfumo. Aidha, usitishaji mapigano unapaswa kuwa hatua ya wazi kuelekea kujiondoa kwa Israel. Mamlaka inayotawala inapaswa kuelewa mateso ya watu wake na kuweka utekelezaji wa usitishaji mapigano kuwa sharti kabla ya kuchukua hatua yoyote nyingine — bila kujali aina yake — ikiwemo kusitisha kile wanachokiita mikutano ya maandalizi na adui. Tunasisitiza kwamba mawasiliano yoyote ya moja kwa moja na adui, kwa aina au jina lolote, hayakubaliki, na inapaswa kuridhika na mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kama ilivyokuwa katika hatua ya awali.

Aliwataka Walebanon wote kushikamana na malengo mawili ya msingi ya kitaifa: kuikomboa ardhi na umoja wa Walebanon; mambo mawili yaliyofungamana kwa karibu, na kufanya uzembe katika mojawapo hakukubaliki, bali inapaswa kuwa msingi wa pamoja ambao kila mtu atasimama juu yake.

Fayyadh alihitimisha kwa kusema: Tunaamini kwamba, aina hii ya fikra na maafikiano juu ya misimamo na juhudi katika njia hii inaweza kusaidia kukabiliana na shinikizo, kusimama imara mbele ya hatari na kufikia malengo.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha